thomnel

Naitwa: Thomas Nelson
Nimezaliwa wa mkoa wa Mbeya.
Nina taaluma ya Mawasiliano ya habari na pia ni mfanyabiashara.
Ninamiliki kampuni mbili. Maranatha Video & General Supplies na Maranatha Perfect clearners, pia ni mwajiriwa wa Taasisi inayoitwa African Malaria Network – Trust ( AMANET)
Mambo !
Nimefurahishwa na suala kuwa wewe ni mjasiriamali, jambo ambalo vijana wengi wa Kitanzania linatushinda ama kwa uoga wa kufanya biashara au kwa sababu ya kukosa mitaji, na wengi tunapenda kuibuka na faida kubwa katika miradi yetu kwa mara ya kwanza badala ya kujifunza kukua taratibu.
Mimi pia ni Mjasiriamali ambaye naendesha ofisi yangu inayoitwa KASEL Employment Solutions, hii inajishughulisha na kutoa ushauri wa kitaalamu katika Sheria za kazi na Utatuzi wa migogoro kazini. Baada ya kumaliza masomo yangu ya shahada ya Mahusiano Kazini nikaona ni vema kama nitatumia taaluma yangu kujiajiri, nina furaha kuwa ninaendelea vizuri.
Nakutakia mafanikio mema kaka !
Asante sana kaka elia. natamani vijana wengi wa kitanzania wangekuwa na moyo kama wako wa kupenda kujiajiri, wengi wanataka kuajiliwa na ajiri ni chache sana, nakutakia mafanikio meme katika shughuli zako. na ninatumai tutafanya kazi pamoja.
Shalom Mh Bwana Mdogo Thom Mwakanyamale,
Hongera sana kwa maamuzi mazuri ya kuwa mjasiliamali mzuri, nimefurahi sana kusikia habari zako njema, bila shaka utakuwa na uzoefu mkubwa sasa!
mi nimechukua nafasi kukupongeza kwani tngu tuachane Mbeya miaka ya tisini mwishoni mwishoni, mpaka sasa nikama miaka 13, ni mingi kiasi chake.
kwa upande wangu sijambo na shemejiako, tunaendelea na ujasiliamali kama nilivo kuambia hapo awali.
wasalaam
E.A Mwaluseke